Watu milioni 850 wanaishi na ugonjwa wa figo. Jibu swali hili la dakika moja ili kujua kama figo zako zina na afya.
Kazi kuu ya figo ni kuondoa uchafu kwa damu na maji ya ziada kutoka kwa damu yako. Figo pia husaidia kudhibiti shinikizo la damu, kuzalisha chembe nyekundu za damu na kufanya mifupa yako kuwa imara. Figo ni viungo vya kushangaza ambavyo hufanya kazi nyingi muhimu ili tuwe na afya. Kiungo hiki ni muhimu sana kiasi kwamba huwezi ishi salama bila figo kufanya kazi. 2
Kati ya asilimia 8 hadi 10 ya watu wazima wana aina fulani ya hitilafu wa figo, na kila mwaka mamilioni hupoteza maisha kutokana na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa figo. 3
Na bado, mtu anaweza kupoteza hadi asilimia 90 ya kazi ya figo kabla ya kupata dalili zozote. 3
Ili kuona kama uko kwa hatari ya kupata ugonjwa wa figo, jibu maswali haya ambayo ni rahisi na yanapatikana ukitumia kiungo cha tovuti iliyooko hapa chini. Kulingana na majibu yako, utapata hatua zinazopendekezwa. Ni vyema uelewe majibu yako na umuhimu wake.
Maswali haya hayakusudiwi kuchukua nafasi ya mashauriano ya matibabu. Ikiwa una mashaka yoyote au maswali, tafadhali zungumza na daktari wako.
Utafiti huu umeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Nephrology kwa usaidizi wa kifedha unaotolewa na AstraZeneca. AstraZeneca pia imetoa usaidizi wa vifaa ili kuunda kurasa za wavuti za uchunguzi.
Maswali ya Figo
Swali la 1 kati ya 7:
Je, umewahi kuambiwa una kisukari?
Maswali ya Figo
Swali la 2 kati ya 7:
Je, umewahi kuambiwa una shinikizo la damu?
Maswali ya Figo
Swali la 3 kati ya 7:
Je, umewahi kuambiwa una ugonjwa wa moyo au kushindwa kufanya kazi kwa moyo?
Maswali ya Figo
Swali la 4 kati ya 7:
Je, mara kwa mara unavimba miguu/mguu au unavimba uso?
Maswali ya Figo
Swali la 5 kati ya 7:
Je, una mwanafamilia ambaye amepandikizwa figo, amekuwa kwenye huduma ya kusafisha figoau kugundulika kuwa na figo inayoshondwa kufanya kazi?
Maswali ya Figo
Swali la 6 kati ya 7:
Je, mara kwa mara unatumia dawa za madukani kwa ajili ya kutuliza maumivu?
Maswali ya Figo
Swali la 7 kati ya 7:
Je, unatumia mara kwa mara dawa za asili, kwa kupunguzauzito au hali nyingine yoyote?
Maswali ya Figo
Matokeo - Sio Hatarini:
Huna sababu zozote za hatari za kupata ugonjwa wa figo lakini bado unaweza kuwa katika hatari.
Sasa tunajua kuna sababu zisizo za matibabu kwa nini watu wanaugua ugonjwa wa figo, ambazo ni pamoja na: 4
- Ambapo mtu anaishi
- Wanapofanyia kazi
- Vyakula wanavyokula
- Wanafanya mazoezi kiasi gani
- Kama wanaweza kupata huduma za matibabu wanayohitaji
JIFUNZE KUHUSU KUZUIA UGONJWA WA FIGO:
Kanuni 8 za Dhahabu za Kinga za Siku ya Figo Duniani
Magonjwa ya figo ni wauaji wa kimya, ambayo kwa kiasi kikubwa yataathiri ubora wa maisha yako. Kuna njia kadhaa rahisi za kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa figo. Angalia Kanuni 8 za Dhahabu!!
Matokeo - Katika Hatari:
UNAWEZA KUWA KATIKA HATARI ZA FIGO ZISIZO NA AFYA
Maelezo Yangu
Umri Wangu:
Jinsia Yangu:
BMI yangu:
1) Je, umewahi kuambiwa una kisukari?
2) Je, umewahi kuambiwa una shinikizo la damu?
3) Je, umewahi kuambiwa una ugonjwa wa moyo au kushindwa kufanya kazi kwa moyo?
4) Je, mara kwa mara unavimba miguu/mguu au unavimba uso?
5) Je, una mwanafamilia ambaye amepandikizwa figo, amekuwa kwenye huduma ya kusafisha figoau kugundulika kuwa na figo inayoshondwa kufanya kazi?
6) Je, mara kwa mara unatumia dawa za madukani kwa ajili ya kutuliza maumivu?
7) Je, unatumia mara kwa mara dawa za asili, kwa kupunguzauzito au hali nyingine yoyote?
Unachoweza Kutaka Kufanya Baadaye
Kulingana na majibu yako, umeonyesha kuwa una mojawapo ya sababu za hatari zinazoweza kusababisha kupungua kwa utendaji kazi wa figo: 4,5,6,7
- Ugonjwa wa kisukari
- Ugonjwa wa Moyo
- Shinikizo la damu
- Historia ya Familia ya Ugonjwa wa Figo, Kupandikizwa kwa Figo, au Kusafisha damu: Watu wana uwezekano wa mara 2 hadi 3 zaidi wa kupata ugonjwa wa figo ikiwa wana wanafamilia walio na ugonjwa wa figo, ambao wamekuwa kwenye dialysis, au wamepandikizwa figo.
- Uzito kupita kiasi: Uzito kupita kiasi unaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kusababisha ugonjwa wa figo
- Kuvimba kwa miguu, au kuwa na uvimbe usoni kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa figo
- Dawa za maumivu zinaweza kudhuru figo zikitumiwa mara kwa mara
- Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za asili yanaweza kudhuru figo
Pia kuna sababu zisizo za kimatibabu ambazo watu hupata ugonjwa wa figo: 5,8
- Mahali Ambapo mtu anaishi
- Wanapofanyia kazi
- Vyakula wanavyokula
- Wanafanya mazoezi kiasi gani
- Kama wanaweza kupata huduma za matibabu wanayohitaji
Kuzungumza na mtaalamu wako wa afya
Mtu anapokuwa na ugonjwa wa figo ina maana kwamba figo zake hazifanyi kazi vizuri kwa sababu figo zimeumizwa na shinikizo la damu, kisukari, au matatizo mengine ya kiafya. 4
Wakati wa kushauriana kuhusu afya ya figo zako, mtaalamu wa afya anaweza kufuata ABCDE Checked - Figo na Moyo zimehifadhiwa:
A = Albumini kwenye mkojo
B = Shinikizo la damu
C = Creatinine na Cholesterol
D = Kisukari (sukari kwenye damu)
E = eGFR
Kulingana na nyenzo za kliniki katika eneo lako, majaribio fulani yanaweza kufanywa: 4,9
- eGFR: Kipimo cha damu ambacho hupima jinsi figo zako zinavyotoa taka kutoka kwa mwili wako
- uACR: Kipimo cha mkojo ambacho hukagua protini inayoitwa albumini
- UPCR: njia ya awali ya kukadiria utolewaji wa protini kila siku kwenye mkojo
- Mtihani wa kukusanya mkojo kwa masaa 24
- Uchambuzi wa mkojo
Baadhi ya maswali unayoweza kuwa nayo kwa mtaalamu wako wa afya ni:
- Je, figo zangu zina afya?
- Je, hivi majuzi nimepimwa ugonjwa wa figo?
- Je, nilipima damu na mkojo?
- Je, nina albumin au protini kwenye mkojo wangu?
- Nifanye nini ili kuweka figo zangu zikiwa na afya?
Maswali mengine muhimu yanaweza kujumuisha:
- Ni nini kitatokea ikiwa nina ugonjwa wa figo?
- Nifanye nini ili kuweka figo zangu kuwa na afya?
- Je, ninahitaji kutumia dawa mbalimbali?
- Je, nifanye mazoezi zaidi?
- Je, ni aina gani ya shughuli za kimwili ninazoweza kufanya?
- Naweza kula nini?
- Je, ninahitaji kuzungumza na mtaalamu wa lishe ili kupata usaidizi wa kupanga chakula?
- Je, ninapaswa kutumia vizuizi vya ACE au ARB* kwa figo zangu?
- Je, ni mara ngapi ninapaswa kuchunguzwa figo zangu?
*Vizuizi vya ACE (vizuizi vya kimeng'enya vinavyobadilisha Angiotensin) na ARB (vizuizi vya vipokezi vya Angiotensin II) ni dawa zinazotumiwa kupunguza shinikizo la damu na/au kupunguza kasi ya kushuka kwa utendakazi wa figo ambayo hutokea kwa ugonjwa wa figo (CKD). 10,11
Figo zako za ajabu:
Figo ni viungo vigumu na vya ajabu ambavyo hufanya kazi nyingi muhimu ili tuwe na afya. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi figo zako zinavyofanya kazi kutoka Siku ya Figo Duniani.
Hadithi za Figo:
Jifunze kutoka kwa watu ote ulimwenguni ambao wamekumbwa na ugonjwa wa figo kwenye blogu ya Siku ya Figo Duniani.
MAMBO AMBAYO HUENDA HUYAJUI KUHUSU UGONJWA WA FIGO.

Zaidi ya watu milioni 850 duniani kote wana aina fulani ya ugonjwa wa figo 12

Kisukari na shinikizo la damu ni sababu kuu mbili za ugonjwa wa figo. 13

Ugonjwa wa figo mara nyingi hauna dalili hadi utakapozidi kuenea, kwa hivyo fanya uchunguzi wa mapema ili ujue hali yako14

Matibabu ya mapema yanaweza kupunguza kasi ya mwendelezo wa ugonjwa 3

Inaweza pia kuzuia matatizo mengine, kama vile mshtuko wa moyo, kiharusi, au kushindwa kazi kwa figo 3,11

Kuwa na ugonjwa wa figo hukuweka katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya kutishia maisha kutoka
COVID-1915
Marejeleo
- WebMD (2018) 850 Million People Worldwide Have Kidney Disease. Available at: https://www.webmd.com/kidney-stones/news/20180705/850-million-people-worldwide-have-kidney-disease. Accessed January 2021.
- National Kidney Foundation. Are you the 33%? Available at: https://www.kidney.org/newsletter/are-you-33-percent. Accessed January 2021.
- World Kidney Day. Chronic Kidney Disease: What is Chronic Kidney Disease? Available at https://www.worldkidneyday.org/about-kidney-health/#whatis. Accessed January 2021.
- Kidney Research UK (2018) Kidney health inequalities in the United Kingdom: Reflecting on the past, reducing in the future. Available at: https://kidneyresearchuk.org/wp-content/uploads/2019/02/Health_Inequalities_Report_Complete_FINAL_Web_20181017.pdf. Accessed January 2021.
- World Kidney Day. 8 Golden Rules. Available at: https://www.worldkidneyday.org/about-kidney-health/#takecare. Accessed January 2021.
- National Kidney Foundation (2014) Prediabetes? What does it mean for your kidneys?. Available at: https://www.kidney.org/news/kidneyCare/Summer10/PreDiabetes. Accessed January 2021.
- McClellan WM, et al (2009) Individuals with a family history of ESRD are a high-risk population for CKD: Implications for targeted surveillance and intervention activities, American Journal of Kidney Diseases, 53(3 S3), pp100-106.
- National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (2016) Preventing chronic kidney disease. Available at: https://www.niddk.nih.gov/health-information/kidney-disease/chronic-kidney-disease-ckd/prevention. Accessed January 2021.
- National Kidney Foundation (2017) Tests to measure kidney function, damage and detect abnormalities. Available at: https://www.kidney.org/atoz/content/kidneytests. Accessed January 2021.
- Kidney Health Australia (2020) Chronic Kidney Disease (CKD) Management in Primary Care, 4th edition. Available at: https://kidney.org.au/uploads/resources/chronic-kidney-disease-management-in-primary-care-4th-edition-handbook.pdf. Accessed January 2021.
- Patient (2017) Chronic kidney disease. Available at: https://patient.info/kidney-urinary-tract/chronic-kidney-disease-leaflet. Accessed January 2021.
- Jager KJ, et al (2019) A single number for advocacy and communication—worldwide more than 850 million individuals have kidney diseases, Kidney International, 96(5), pp1048-1050.
- WebMD. Kidney Disease. Available at: https://www.webmd.com/a-to-z-guides/understanding-kidney-disease-basic-information#1. Accessed January 2021.
- NHS England (2019) Overview: Chronic kidney disease. Available at https://www.nhs.uk/conditions/kidney-disease/. Accessed January 2021.
- Centers for Disease Control and Prevention (2020) COVID-19 (Coronavirus): People with Certain Medical Conditions. Available at: https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-ncov/need-extra-precautions/people-with-medical-conditions.html#chronic-kidney-disease. Accessed January 2021.
- National Kidney Foundation (2014) 10 Signs You May Have Kidney Disease. Available at: https://www.kidney.org/news/ekidney/august14/10_Signs_You_May_Have_Kidney_Disease Accessed October 2021
- National Kidney Foundation (2021) Herbal Supplements and Kidney Disease. Available at: https://www.kidney.org/atoz/content/herbalsupp Accessed October 2021
